Toleo la Wiki: Dashibodi ya Jamii ya Common Voice imerudi na zaidi

TLDR: Toleo la Jumatano kwenye Mfumo wa Common Voice, Mawazo tofauti ya Lugha kwenye Common Voice, Dashibodi ya Jamii imerudi!

:sparkling_heart: Heri ya Mwaka Mpya wa Mwezi Mpya! Kwa wanajamii wanaosherehekea

Dashibodi ya Common Voice ya Jamii

Tumepokea maombi mengi kuhusu kuwa na uchanganuzi wazi wa umma kwa Common Voice. Huu ni mradi unaoendelea, lakini kama hatua ya kwanza sasa unaweza kuona takwimu kadhaa muhimu - ikiwa ni pamoja na wachangiaji wapya, klipu za kila siku, lugha kuu kwa saa na zaidi - kwenye dashibodi hii ya Grafana.

Tazama maelezo yetu ya hivi punde kuhusu toleo ya jukwaa kwenye github yetu.

Shiriki katika kuanzisha vibadala vya Lugha kwenye Common Voice

Tunataka kuifanya Common Voice ijumuishe zaidi kiisimu na tutaanzisha vibadala mwishowe mwa Q1.

Vibadala(/Lahaja): Aina maalum ya lugha au kikundi cha lugha inayohusishwa na kundi la wazungumzaji, kwa mfano wale wanaoishi katika eneo au nchi, au ambao wana utamaduni au turathi sawa, na kwa hivyo huwa na msamiati, sarufi na kanuni zinazotofautisha usemi wao kutoka kwa wengine.

*Kumbuka kwamba sisi hutumia neno vibadala badala ya lahaja kwa sababu lahaja, saa zingine, imetumiwa kwa njia za kudhalilisha, hata hivyo vibadala havidhibitiwi kijiografia pekee.

Rejelea: Jinsi tunavyoifanya Common Voice iwe inajumuishi zaidi kiisimu, blogi na Timu ya Common Voice

Asante kwa jamii ambaza kufikia sasa zimeshiriki maoni yao kuhusu vibadala vya lugha yao kupitia utafiti wetu na mazungumzo ya 1:1.

Tunataka kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma kwa hivyo tumeongeza wakati wa uchunguzi wa raundi ya kwanza. Iwapo jumuiya yako ya lugha inataka kushiriki tafadhali angalia mwongozo wetu na ukamilishe utafiti kabla ya tarehe 10 Februari.

Fursa na Vifijo

  • List item FOSDEM ni wiki hii! Njoo na uunge mkono Bulent, Micheal na Saverio ambao wanawasilisha mazungumzo kuhusu Common Voice mnamo tarehe 5 Februari.

  • List item Mozfest inakaribia hivi karibuni! Angalia ratiba na ujiandikishe kuhudhuria. Unaweza kujiandikisha bila malipo au kulipa unachoweza.

  • List item Je, ungependa kuunda programu ya utambuzi wa usemi kwa kutumia sauti yako mwenyewe? Ikiwa ndio, angalia mafunzo haya yaliyoandaliwa na Coqui, yaliyoangaziwa kwenye blogi yetu.

Kila la kheri,
Kat.