TLDR: Tunakaribisha wanachama wapya kwenye Timu ya Common Voice na kuchapisha mwongozo, kwa jamii, ya kuanzisha vibadala vya lugha.
Hujambo Jamii ya Common Voice,
Asante sana kwa maoni yenu kuhusu muundo mpya wa ‘ukurasa wa kuhusu’. Toleo la wiki hii linahusisha utambulisho wa wanachama wapya na mwongozo, kwa jamii, wa vibadala.
Kuanzisha vibadala vya Lugha kwenye Common Voice
Mwaka jana, tulichapisha mkakati wetu wa kufanya Common Voice ijumuishe zaidi kiisimu.
Ili kufanya hii iwezekane tunahitaji ushiriki wako. Tunaalika jumuiya kushiriki katika kupendekeza vibadala ambavyo wangependa kuungwa mkono.
Tumeunda baadhi ya [miongozo](https://common-voice.github.io/community-playbook/sub_pages/Lang_Variant.html) ili kusaidia jumuiya katika kuwasilisha vibadala vya lugha zao. Tafadhali soma miongozo kikamilifu kisha jadili na vikundi vyenu vya jumuiya. Pindi jumuiya yako ya lugha imejadili na kuamua ni vibadala vigani mngependa kutumia, [tafadhali wasilisha chaguo lenu kupitia fomu hii ya google](https://forms.gle/gkVyYzai2cUmNUTW8) kabla ya tarehe 31 Januari 23:00 UTC.
Msaada Zaidi
- Tuna kikao cha ‘Niulize Chochote’ pamoja na Francis kuhusu Vibadala vya Lugha kwenye Common Voice. Unaweza kuwasilisha maswali mapema.
- Unaweza pia kufikia Francis kupitia Matrix
Wanachama Wapya wa Timu ya Common Voice
Wiki hii Timu ya Common Voice ilikaribisha washiriki watatu wapya. Tafadhali wakaribishe kwa uchangamfu na fadhili.
@zaccolley - Zac anajiunga kama msanidi programu kamili anayelenga safu ya mbele. Wanavutiwa na ufikiaji wa wavuti, utendaji, kuandika juu yao wenyewe katika mtu wa tatu
@gzh - Gabriel amekuwa shabiki wa mambo yote ya Mozilla kwa muda mrefu, anajiunga na timu ya Common Voice kama msanidi programu kamili anayezingatia safu ya nyuma.
@sabrinang — Sabrina, Mbunifu wa Uzoefu wa Mtumiaji na Kiolesura (UX/UI) kwenye timu ya Mozilla Foundation ya Ushiriki wa Kidijitali ambaye atafanya kazi na timu ya Common Voice.
Fursa na Matukio
- Je, unahitaji usaidizi na wazo kuhusu jumuiya yako? Unaweza kupata usaidizi kwenye Dawati la Usaidizi kwa Jamii tarehe 2 Alhamisi, Januari 20, 11 asubuhi UTC na 2pm UTC
- 2022 ni mwanzo wa Muongo wa UN wa Mataifa kwa Lugha za Asili. Tamasha la Lugha za Asili (Jan 14 hadi 23). Mkusanyiko wa mtandaoni wa kusherehekea na kutunganisha mwanzoni mwa Muongo wa Kimataifa wa Lugha za Asili 2022-2032!
- Chapisho jipya la blogu na Kathleen “Katika kutayarisha makala za blogi ambayo tunachapisha kwenye lugha ya sw na pia en, nimejipata nikifanya tafsiri ya makala. Nikawa na hamu kujua jinsi tafsiri ya Google Translate ingelingana na yangu.” soma zaidi kwenye blogu.
Ikiwa una maswali yoyote tafadhali kuwa huru kuuliza.
Kila la heri,
Kat.