Toleo la Wiki: Hifadhidata ya Common Voice ijayo na mengine

:fireworks:
Heri ya Mwaka Mpya!

Kwa toleo letu la kwanza katika mwaka wa 2022, tunashughulikia, tokeo la hifadhidata ya Common Voice ijayo, fursa, matukio na maazimio ya mwaka mpya!

:star2:
Hifadhidata ya Common Voice ijayo

Hifadhidata ya Common Voice inatolewa mwezi huu. Hifadhidata imeongezeka kwa takriban saa 5,000 zilizorekodiwa :boom: , juhudi zako zilisaidia hii kuwezekana.

Kuthibitisha rekodi za sauti husaidia kuboresha hifadhidata ya Common Voice ili programu inayoundwa kwa kutumia hifadhidata iweze kuelewa watu vyema.

Kipindi cha kujumuisha rekodi za sauti kwa toleo lijalo kimepangiwa Januari 12.

Je, unaweza kusaidia kuthibitisha rekodi za sauti kabla ya toleo la mwezi huu?

Kama ndiyo ! shiriki katika changamoto ndogo ya 5x15. Katika siku 5 zijazo, thibitisha rekodi za sauti kwa dakika 15 kila siku.

Uko huru kutumia tena gif na nina furahi kutengeneza matoleo yaliyojanibishwa kwa watakaoomba kupitia ujumbe wa moja kwa moja.

:speech_balloon:
Fursa na Matukio

  • Shiriki mawazo yako kuhusu muundo mpya na maudhui ya Ukurasa wa Kuhusu kwenye Sauti ya Kawaida (mkato wa Jumatatu, tarehe 10, 10am UTC)
  • Changia muundo wa Dawati la Usaidizi kwa Jamii. Dawati la Usaidizi linalenga kusaidia jamii zinazotaka kuona lugha yao ikikua kwenye Common Voice.
  • Kikao cha ‘Niulize Chochote’ pamoja na Francis kuhusu Vibadala vya Lugha kwenye Common Voice inayofanyika Januari tarehe 24.
  • FOSDEM inafanyika tarehe 5 na 6 Februari. Mozilla inapanga devroom, angalia ajenda na uje kuwaunga mkono Mozillians wenzako.

:goal_net:
Maazimio ya Mwaka Mpya

Ungependa kutengeneza maazimio gani ya mwaka mpya?

Inaweza kuwa …

Kila la heri,
Kat.